Sababu mahusiano yanapoteza uelekeo:
1. Kazi
Wote ni wafanyakazi. Mpo bize sana hamna muda wa kukaa pamoja kuongea au kutoka out
2. Watoto.
Mke umezaa juhudi zako zote ni kwenye malezi unamsahau mume.
Mume hujihusishi na malezi ya watoto wako unamuachia mke ambae malezi ya peke yake yanamchosha.
3. Starehe
Kuendekeza starehe mpaka inafikia unamuona mwenzi wako mzigo.
4. Kutokujali
Kutojihusisha na shughuli anazofanya mwenzi wako kiasi anakuwa na mchepuko huna habari.
Kutokushirikiana/not sharing, kila mtu anafanya yake.
Hamuwezi kusema mnapendana kama ya hapo juu mnayaruhusu kwenye mahusiano yenu.